Sumbawanga. Polisi wilayani hapa inamshikilia mkazi wa Kijiji
cha Lwanji, Bonde la Ziwa Rukwa, Edwin Kachele (30) kwa tuhuma ya
kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 11 kwa kile kinachodaiwa kuwa ni
imani za kishirikina.
Mtoto huyo (Jina linahifadhiwa) anadaiwa kufanyiwa
kitendo hicho Agosti 11, saa 2:00 usiku nyumbani kwao wakati mama yake
alipokuwa ameenda kunywa pombe katika moja ya nyumba zilizo jirani na
nyumbani kwake.
Akisimulia mkasa huuo, kaimu kamanda wa polisi wa
Mkoa wa Rukwa, Ferdinand Rwegasira alidai kuwa majirani walisikia kelele
za mtoto huyo akiomba msaada, walipofika walimkuta Kachele akimfanyia
ukatili huo binti yake. Walimkamata na kumfikisha Kituo cha Polisi
Mtowisa.
Inadaiwa mtuhumiwa alifanya kitendo hicho baada ya
kupewa masharti na mganga wa kienyeji kuwa alale na mabinti zake ambao
ni mabikira, atakuwa tajiri.
Rwegasira alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wiki ijayo.