Saturday 2 April 2016

Trump ‘ajipendekeza’ kwa wakuu Republican

Mgombea urais anayeongoza katika chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amechukua hatua ya kushangaza akijaribu kuimarisha uhusiano uliodorora kati yake na wakuu wa chama hicho.

Mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York ametembelea Kamati Kuu ya Taifa ya Republican.
    Trump ayumbayumba kuhusu utoaji mimba

Amechukua hatua hiyo siku moja baada ya kuwakera viongozi hao kwa kusema kwamba hatatii makubaliano ya kuunga mkono mgombea mwengine, iwapo yeye mwenyewe hatashinda uteuzi wa chama hicho.

Bw Trump, anayeongoza kwa wajumbe kwa sasa, amekosoa kile anachosema ni juhudi zisizo za kidemokrasia za kutaka kumpkonya ushindi katika mkutano mkuu wa kuidhinisha mgombea mjini Cleveland mwezi Julai.

Paul Makonda aahidi neema kwa waendesha bodaboda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekutana na waendesha pikipiki za kubeba abiria maarufu kama Bodaboda mkoani Dar na kuwapa ahadi nono za kuwainua kimaisha kupitia biashara hiyo.

Pamoja na mambo mengine, Makonda ameahidi kuwapa pikipiki bodaboda hao kwa marejesho ya shilingi 25,000 kwa wiki (sawa na shilingi 3,500) kwa siku na baadae kuwaachia wazimiliki wao.

Katika hatua nyingine, Makonda ameahidi kuwatengenezea mpango mzuri  utakaowawezesha bodaboda hao kuingia katikati ya Jiji, tofauti na ilivyo sasa.

Mwakilishi wa Bodaboda, Daud Laurian alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni zuio la kuingia mjini (CBD) la Machi 3,2014.
“Tumekutana na changamoto nyingi, kwa mfano kutozwa faini kuanzia Sh50,000 hadi zaidi ya 400,000, kukamatwa kinyama na kufukuzwa na magari,” alisema.

Ahadi ya Makonda kuwaruhusu Bodaboda kuingia Jijini ni ukamilifu wa ahadi ya Rais John Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.

Juzi, Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Chadema) pia aliahidi kuhakikisha Bodaboda wanaweza kuingia mjini kwa utaratibu maalum.

Polisi Jijini Mwanza Waamuru Kaburi la Marehemu Lifukuliwe

Polisi mkoani Mwanza, ndugu, jamaa na marafiki, juzi, walilazimika kufukua kaburi na kutoa mwili wa Gelinde Masumbuko baada ya kuzikwa na ndugu wa marehemu Said Mussa na kukaa kaburini kwa siku mbili.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Mwanza wa Sekou-Toure, kuukabidhi mwili wa Masumbuko kwa ndugu wa Mussa.

Baada ya kukabidhiwa mwili huo, ndugu wa Mussa waliendelea na taratibu na kuuzika katika makaburi ya Nyashana wilayani Ilemela, kabla ya ndugu wa Masumbuko kubaini kuwa mwili wa ndugu yao uliokuwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hauonekani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alisema walilazimika kuingilia kati suala hilo baada ya ndugu wa Masumbuko kuripoti tukio la mwili wa ndugu yao kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

“Baada ya uchunguzi kwa kushirikiana na uongozi wa hospitali tulibaini yalifanyaka makosa kwa mwili huo kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu Mussa ambao tayari walishauzika,” alisema.

Uchunguzi huo ulibaini mwili wa Mussa ulikuwa bado umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo.
“Ilibidi taratibu za kisheria zichukuliwe na mwili wa marehemu Masumbuko kufukuliwa na kukabidhiwa kwa ndugu zake, huku ndugu wa Mussa nao wakichukua mwili wa ndugu yao kwa mazishi mapya,” alisema Kamugisha.

Mkanganyiko huo ulitokea baada ya ndugu wa Masumbuko kutoka Sengerema kufuata mwili katika hospitali hiyo na kuukosa, hali iliyowalazimu kufuatilia ili kujua alikozikwa na taratibu za kuufukua zifuatwe.

Ndugu wa Masumbuko, Finias Elias, alisema walitarajiwa kumzika jana nyumbani kwao wilayani Sengerema.
Ndugu wa marehemu Mussa, Said Mussa alisema waliotumwa kuuchukua mwili wa marehemu walishindwa kumtambua kutokana na kuvimba uso.

Friday 5 September 2014

Ajali Mbaya Ambayo Haijawai Kutokea Musoma,Na Kusababisha Fiesta Kuahirishwa Mkoani Hapa

Ni ajali mbaya kuwahi kutokea katika mkoa wa Mara...Ni ajali iliyotokea leo asubui mida ya saa nne asubuhi ambapo basi la J4 lilokuwa likitoka Mwanza kwenda tarime limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza Coach ambalo lilikuwa likitoka Musoma likienda Mwanza.

Chanzo cha ajali hiyo ni gari ndogo aina ya Land Cruiser ambayo ilikuwa ikiovatek bas la J4 ndipo baada ya kupoteza uelekeo kwenye kona ilioko maeneo ya sabasaba %ziro ziro% na kuacha mwanya wa basi hizo mbili kupoteza uelekeo na kugongana uso kwa uso.

Mpaka kufikia sasa watu waliofariki katika ajali hiyo ni 70 ambapo bas la J4 limeuwa abiria wote na majeruhi wa mwanza coach ni wengi pia.

Mungu zilaze mahali pema roho hizo

Sunday 17 August 2014

BABA AMBAKA MWANAYE WA KUMZAA AKITAFUTA UTAJIRI


Sumbawanga. Polisi wilayani hapa inamshikilia mkazi wa Kijiji cha Lwanji, Bonde la Ziwa Rukwa, Edwin Kachele (30) kwa tuhuma ya kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 11 kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina.

Mtoto huyo (Jina linahifadhiwa) anadaiwa kufanyiwa kitendo hicho Agosti 11, saa 2:00 usiku nyumbani kwao wakati mama yake alipokuwa ameenda kunywa pombe katika moja ya nyumba zilizo jirani na nyumbani kwake.
 
Akisimulia mkasa huuo, kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Rukwa, Ferdinand Rwegasira alidai kuwa majirani walisikia kelele za mtoto huyo akiomba msaada, walipofika walimkuta Kachele akimfanyia ukatili huo binti yake. Walimkamata na kumfikisha Kituo cha Polisi Mtowisa.
 
Inadaiwa mtuhumiwa alifanya kitendo hicho baada ya kupewa masharti na mganga wa kienyeji kuwa alale na mabinti zake ambao ni mabikira, atakuwa tajiri.
 
Rwegasira alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wiki ijayo.

Thursday 14 August 2014

PICHA ZA MAZISHI YA MKE WA MSANII AFANDESELE

 Msanii wa miondoko ya hip hop nchini Afande Sele hapo usiku wa jana alipata pigo kubwa la kufiwa na mzazi mwenzake (mke wake)  akizungumza na Mwarick blog Afande Sele alisibitisha kifo cha mke wake huyo na kusema "KWELI NIMEFIWA NA MKE WANGU USIKU HUU HATA SIELEWI TATIZO NINI" Alisema Afande huku akilia kwa uchungu.
 Kutokana na kanuni za Dini ya KIislam maherehemu amezikwa leo huko mkoani Morogoro.

"Timu nzima ya Mwarick blog inatoa pole kwa wafiwa wote walio kutwa na msiba huo"

TAZAMA PICHA ZA MSIBA HUO HAPA

ASANTE KWA KUWA NASI