Sunday 17 August 2014

BABA AMBAKA MWANAYE WA KUMZAA AKITAFUTA UTAJIRI


Sumbawanga. Polisi wilayani hapa inamshikilia mkazi wa Kijiji cha Lwanji, Bonde la Ziwa Rukwa, Edwin Kachele (30) kwa tuhuma ya kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 11 kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina.

Mtoto huyo (Jina linahifadhiwa) anadaiwa kufanyiwa kitendo hicho Agosti 11, saa 2:00 usiku nyumbani kwao wakati mama yake alipokuwa ameenda kunywa pombe katika moja ya nyumba zilizo jirani na nyumbani kwake.
 
Akisimulia mkasa huuo, kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Rukwa, Ferdinand Rwegasira alidai kuwa majirani walisikia kelele za mtoto huyo akiomba msaada, walipofika walimkuta Kachele akimfanyia ukatili huo binti yake. Walimkamata na kumfikisha Kituo cha Polisi Mtowisa.
 
Inadaiwa mtuhumiwa alifanya kitendo hicho baada ya kupewa masharti na mganga wa kienyeji kuwa alale na mabinti zake ambao ni mabikira, atakuwa tajiri.
 
Rwegasira alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment