Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda amekutana na waendesha pikipiki za kubeba abiria maarufu
kama Bodaboda mkoani Dar na kuwapa ahadi nono za kuwainua kimaisha
kupitia biashara hiyo.
Pamoja na mambo mengine, Makonda
ameahidi kuwapa pikipiki bodaboda hao kwa marejesho ya shilingi 25,000
kwa wiki (sawa na shilingi 3,500) kwa siku na baadae kuwaachia
wazimiliki wao.
Katika hatua nyingine, Makonda ameahidi
kuwatengenezea mpango mzuri utakaowawezesha bodaboda hao kuingia
katikati ya Jiji, tofauti na ilivyo sasa.
Mwakilishi wa Bodaboda, Daud Laurian alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni zuio la kuingia mjini (CBD) la Machi 3,2014.
“Tumekutana na changamoto nyingi, kwa
mfano kutozwa faini kuanzia Sh50,000 hadi zaidi ya 400,000, kukamatwa
kinyama na kufukuzwa na magari,” alisema.
Ahadi ya Makonda kuwaruhusu Bodaboda
kuingia Jijini ni ukamilifu wa ahadi ya Rais John Magufuli wakati wa
kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.
Juzi, Meya mpya wa Jiji la Dar es
Salaam, Isaya Mwita (Chadema) pia aliahidi kuhakikisha Bodaboda wanaweza
kuingia mjini kwa utaratibu maalum.
No comments:
Post a Comment