Mgombea urais anayeongoza katika
chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amechukua hatua ya
kushangaza akijaribu kuimarisha uhusiano uliodorora kati yake na wakuu
wa chama hicho.
Mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York ametembelea Kamati Kuu ya Taifa ya Republican.
Trump ayumbayumba kuhusu utoaji mimba
Amechukua hatua hiyo siku moja baada ya
kuwakera viongozi hao kwa kusema kwamba hatatii makubaliano ya kuunga
mkono mgombea mwengine, iwapo yeye mwenyewe hatashinda uteuzi wa chama
hicho.
Bw Trump, anayeongoza kwa wajumbe kwa
sasa, amekosoa kile anachosema ni juhudi zisizo za kidemokrasia za
kutaka kumpkonya ushindi katika mkutano mkuu wa kuidhinisha mgombea
mjini Cleveland mwezi Julai.
No comments:
Post a Comment